ADVERTISE WITH US

Maadhimisho siku ya uvuvi duniani kufanyika Mafia

Tanzania inaweza kunufaika na utalii wa samaki aina ya papa potwe waliorejea katika pwani ya Bahari ya Hindi baada ya kutoweka kutokana na uharibifu wa mazingira.



Akizungumzia maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani yafanyikayo leo Jumanne Novemba 20,2017 kisiwani humo, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyama (WWF ), Dk Amani Ngusaru amesema papa potwe 100 wamerejea.

Dk Ngusaru amesema jana Jumatatu Novemba 20,2017 kuwa sifa ya samaki hao ni ukubwa wao unaofikia uzito wa kati ya tani 15 na 22, urefu wa mita 12, rangi na upole unaowafanya watalii kuweza kuwasogelea.

"Katika maadhimisho ya mwaka huu tunamuenzi papa potwe kwa sababu anabeba sifa ya kisiwa cha Mafia, tunatarajia kuzindua mnara wa sanamu ya samaki kama alama pekee kisiwa hapa," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Anunduma amesema Serikali ya wilaya imeanza kuonja utajiri unaotokana na uwepo wa samaki hao. Amesema wameutambua umuhimu wake na msisitizo kwa sasa ni kuendelea kuhifadhi mazingira na kupambana na uvuvi haramu ili wasitoweke tena.

"Niwaombe wadau wote tusaidiane kuutangaza utalii huu muhimu kwa uchumi wetu, kisiwa hiki kinaweza kutajirika kwa sababu tu ya hawa samaki," amesema.

Mratibu wa utunzaji wa rasilimali za bahari wa WWF, Dk Mathias Igulu amesema katika maadhimisho yatakayoongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wananchi, wakiwemo wavuvi watapata nafasi ya kumfahamu samaki huyo kwa undani na kuona umuhimu wa kumtunza.

Dk Igulu amesema kwa sababu samaki hao hawapendi bugudha, wanaweza kutoweka iwapo uvuvi haramu wa kutumia baruti na uharibifu wa mazingira utaendelea.

No comments: