ADVERTISE WITH US

ZIJUE APPS 5 ZA ANDROID ZENYE UWEZO WA KUTAMBUA NYIMBO


Umeshawahi kusikia ngoma kali, ukaipenda, ukataka kuimiliki na ukataka kuwatumia marafiki..Lakini ukagundua haufahamu wimbo wala msanii? Usiwaze.
 Kupitia Simu Janja yako unaweza kupakua App ambayo inaweza kukusaidia kupata ufumbuzi wa ishu hiyo.
App Hiyo inaweza kukusaidia kujua jina la msanii, Jina la Wimbo au hata Jina la Albamu, kwako inatakiwa kufanya ni Kuisogeza Simu yako karibu na Spika zinazopiga wimbo huo husika, unarekodi kisha unaelekea katika App mojawapo kwaajili ya utambuzi.


Shazam
Katika moja ya App bora katika utambuzi wa nyimbo, Hii iko poa sana. Ikiwa tayari imepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 100 duniani kote. Shazam husaidia kutambua wimbo unaousikia kutokea katika Radio, Televisheni au hata Kompyuta Yako.

Unachotakiwa kufanya ni kufungua Programu, kisha kuisogeza simu yako karibu na spika zinazopika wimbo Husika.


Ndani ya Sekunde chache tu, itakupatia Jina la wimbo, la msanii, la albamu ( Kama ipo) na kukupa viunganishi vya kuipata, kama ni Youtube au mitandao mingine.

SoundHound
Hii ni mojawapo ya Programu pia bora katika utambuzi wa Wimbo unaohitaji. Inapatikana pia bure, uzuri wa hii imeenda mbali zaidi ambapo Inaweza kutambua wimbo hata wewe Ukiimba tu.


Track ID
App hii inamilikiwa na Sony Mobile Communication. Kitu kizuri kuhusu App hii ni kuwa, inapatikana katika kwa lugha zaidi ya 60.


Kama ilivyo Shazam, nayo inafanya kazi hivyo hivyo.

What’s That Song?

Kwa hapa, App Hii inaendelea kuthibitisha uchawi wa Teknolojia. Yenyewe unahitaji kuzungumza maneno kadhaa ambayo ulikuwa umeyashika katika Wimbo Huo na sio kuimba, ambapo App hii itafanya kukuleta nyimbo kadhaa zinazoendana na kile ulichokisema kwenye kinasa sauti cha Simu yako.
Identify Music

Kama kawaida hii nayo inakupa majibu ndani ya Sekunde chache sana. Hii hufanya kazi kwa kuisikilizisha Simu yako wimbo unaohitaji kujua. Na haiishii kukupa jina la wimbo, msanii na albamu bali inakupa hata mapendekezo ya Nyimbo nyingine ambazo zinaendana na hiyo.

No comments: