ADVERTISE WITH US

ORODHA YA NYIMBO ZILIZOPO KATIKA ALBAMU YA J. COLE ''K.O.D''


Albamu mpya ya J. Cole "K.O.D" itatolewa siku ya Ijumaa na Kava la Album hii  sasa linapatikana.    Albamu mpya inakuja na nyimbo 12 ikiwa ni pamoja na Intro, kuna nyimbo mbili kafanya  msanii mgeni kwenye albamu hii anaekwenda kwa jina la Kill Edwards.
Nini maana ya jina la "K.O.D"? bado haijulikani lakini moja ya majina ya kazi yamekuwa  “Kids On Drugs” na watu wanajuaji kutokana na michoro ambayo ipo katika Kava la Albamu. J. Cole hivi karibuni alifungua Instagram kwa machapisho yake yote ya awali kabla ya kutangaza kuwa anaacha albamu mpya kwenye show ya bure ya pop up mjini New York Jumatatu usiku.

 Rapa kutoka Dreamville alikimbiza mtandaoni na tangazo lake la albamu, ishara za wazi zinatibitisha kuwa yeye ni mojawapo ya majina makubwa kwa sasa. Ni wasanii wachache pekee ambao wanaweza kusababisha frenzy sana na tangazo la albamu na hawa ni pamoja na, Drake, Kendrick Lamar, Beyonce, na JAY-Z.

soma pia👉 J. COLE KUJA NA ALBAMU MPYA WIKI HII

 Wakati huu hatumjui Kill Edwards ni nani lakini vyanzo vinasema Kill Edwards ni mwanachama wa lebo ya Dreamville ya J. Cole. Hata hivyo, tutajua ni nani Ijumaa wakati albamu itakapo achiwa. Cole inawezekana kwenda kwenye ziara ili kukuza Project hiyo, lakini hadi sasa hakuna kitu kilichotangazwa.

K.O.D. tracklist:

1. Intro
2. K.O.D
3. Photograph
4. The Cut Off ft. Kill Edward
5. ATM
6. Motives
7. Kevin’s Heart
8. BRACKETS
9. Once An Addict (Interlude)
10. FRIENDS ft. Kill Edward
11. Window Pain (Outro
12. 1985 (Intro To The Fall Off)

 

No comments: