ADVERTISE WITH US

J COLE : "ALBAMU YANGU YA K.O.D INANIKUMBUSHA NILIPOTEMBELEA ZANZIBAR,TANZANIA"

Tarehe 20/ April 2018 Msanii wa Hip Hop na producer Jermaine Lamar Cole almaarufu J Cole anatokea kwenye viunga vya Fayettevile, North Carolina, Marekani. Alitoa Album yake ya tano iitwao KOD yenye kirefu cha Kids On Drugs, Kill Our Demons au King Overdose.
Ndani ya Album hii KOD amezugumzia kuhusu tatizo la madawa ya kulevya na jinsi ya kuhandle maumivu ya maisha bila kutumia njia hatarishi km za Madawa au kujiigiza starehe zisizostahili km Xanny. J. Cole amethibitisha hilo jana Aprili 27, 2018 kwenye ukurasa wake wa Twitter akijibu maswali ya mashabiki wake ambapo moja ya mashaabiki aitwae Zion alimuuliza “Jina la album yako ulilipata baada au kabla ya kumaliza kurekodi?”.

J. Cole alimjibu shabiki huyo kwa kumwambia kuwa While in Zanzibar workin' on one of the songs, maybe window pain, I asked myself what is the name of this album that I just fucked around and made. KOD came immediately. "What the f*ck do that mean?" I asked. the 3 meanings followed in seconds. In tune. akimaanisha (“Wakati nikiwa Zanzibar nikirekodi baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album. Nilijiuliza album hii nitaipa jina gani? lakini ghafla nikajikuta naipa jina hilo (KOD). Swali nililojiuliza jina hilo lina maana gani?.Lakini baadae nikapata maana tatu ya jina hilo na kuziweka kwenye wimbo.)
Pia amezitaja nyimbo 4 kati ya 12 alizifanya akiwa Tanzania, Zanzibar nyimbo alizo ziandika akiwa Tanzania ni The Cut off, Kevin's Heart, FRIENDS na Window Pain. Nyimbo zingine zinazopatikana kwenye Album hii ni Photograph, 1985, Moti8, BRACKETS, ATM, Once an Addict na Intro
pia amefunguka kuwa ’Memory’ nzuri zaidi wakati anaandaa album yake mpya ya ‘KOD’ ni Zanzibar, Tanzania.  Kwa wale walioisikiliza hii Album mtakubaliana nami ndie Album bora kutoka kwa J. Cole ukisikiliza nyimbo zote pamoja na ujumbe uliopo kwenye izo nyimbo haina ubishi hii Album bora ikifatiwa na 2014 Forest Hill Drive halafu Born Sinner, 4 Your Eyez Only then Cole World :The Sideline Story.
 Unaweza ukasikiliza wimbo huo wa Window Pain ambao umeeleza maana ya jina la ‘KOD’ .

No comments: