Msanii
Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini
(kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa
kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba
wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours.
Wimbo
huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani,
Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa
na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine
chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha
kupata fursa ya kushiriki kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa
ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau
tasnia ya muziki kwa ujumla.
“Kwangu
hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa
kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki
kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata
umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond.
Kwa
upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo,
alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano
haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini
Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani
watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya
mashindano haya”alisisitiza.
Prodyuza
nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye
ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa
jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa
nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa.
“Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika
tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima
kubwa tuliyopewa”


No comments:
Post a Comment