TOANGOMA, NI TOANGOMA KWELI?
Toangoma ya sasa ni miongoni mwa maeneo maarufu sana ya Dar es Salaam.
Umaarufu huu unatokana na uwepo wa miundombinu bora ya kimakazi na mpangilio wa mitaa yake.
Toangoma ina mtaa maarufu wa Masaki ambao unaelekeza ilipo stendi kuu ya eneo hili la Toangoma, mtaa huu umejengeka vilivyo.
Wengi tunalifahamu jina hili la Toangoma, lakini huenda hatufahamu jina hili limetokeaje.
Jina Toangoma limetokana na wenyeji wa Dar es Salaam (Mzizima) kwa maana ya Wazaramo wa miaka ya kale ambao walikuwa wakitoka maeneo mengine ya uliokuwa Mkoa wa Pwani kama vile Kimbiji, Puna, Mwembe Mgodo, Kijiji cha Ujamaa Gezaulole, Mjimwema, Mwembe Mtengu na mengineyo ambao walikuwa wakikutana eneo hilo huku wakiwa na ngoma zao kwa ajili ya kuja kukutana na wenzao wa Mtoni kwa Aziz Ally, Buguruni na kwingineko.
Walipokuwa wakifika eneo hili la Toangoma walikuwa wakitua ngoma zao na kuweka kambi kwa muda. Walikula na kupumzika hapo kabla ya kuanza safari yao.
Kutokana na mazoea ya kukutana eneo hilo na "kutua" yaani kushusha ngoma zao kwa ajili ya mapumziko eneo hilo likajulikana kwa jina la "TUANGOMA".
Kadiri miaka ilivyosonga na muingiliano wa kijamii utamkaji wa 'Tuangoma' ulibadilika na kuwa 'Toangoma'.
Hivi ndivyo neno Toangoma lilivyotoholewa kutoka Tuangoma na kuwa Toangoma tunayoifahamu leo.
Chanzo : Kona ya Wahenga.

No comments:
Post a Comment