Mara nyingi tumekuwa tukiwasikia waigizaji kama Kelvin Hart, Madea au Martin Lawrence wakizungumza lugha ambayo wengi wetu huwa ni ngumu kuielewa kwa kiasi fulani.
Lugha wanayoongea inaitwa Ebonics! Lugha hii inaongewa na Waamerika wengi weusi. Ebonics inatokana na maneno "Ebony" lenye maana ya 'Black' yaani 'Nyeusi' na "Phonics" lenye maana ya 'Sound' yaani 'Sauti.'
Neno Ebonics lilianzishwa mwaka 1973 na kundi la Wasomi waamerika weusi ambao hawakupendezwa na jina lililokuwa likitumiwa la "Nonstandard Negro English" ambalo lilitumika kuanzia miaka ya 1960 wakati elimu juu ya lugha hiyo ilipoanzishwa.
Baadae mwaka 1996 Bodi ya Lugha ya Shule ya Oakland iliitambua lugha hii kama lugha ya msingi ya waamerika wenye asili ya Afrika.
Lugha hii mashuleni na vyuoni hujulikana kama "African American English" (AAE) au "African American Vernacular English" (AAVE) kutokana na utamkaji wake kuwa na athari ya lugha za kiafrika toka nchi kama Nigeria, Ghana n.k
Waamerika wengi weusi hawawezi kuzungumza "Standard English" hivyo huwapasa kwenda darasani kufundishwa.
Ebonics "siyo Slang!". Slang hutumiwa zaidi na vijana na wanahiphop na rap. Mfano wa maneno ya slang ni kama " Blingbling" ambalo humaanisha 'Glittery, expensive jewelry " na lingine kama "phat" likimaanisha 'Excellent'.
Ebonics ina maneno kama han (hand), mah rahd (my ride) bah (but).
Msikilize Kelvin Hart na Madea utasikia Ebonics.






No comments:
Post a Comment