Vijana wengi wa Dar es Salaam leo hii ukiwauliza "Unapafahamu MWEMBETOGWA?" watabaki wanakuangalia tu kwa mshangao.
Sasa kuanzia leo noamba mfahamu kuwa sehemu ambayo siku hizi inajulikana kama "Fire" au 'Faya' pale ambapo kuna traffic lights zinazoongoza gari za kwenda/kutoka Kariakoo kuelekea Muhimbili na kwenda/kutoka Jangwani/Magomeni kuelekea Posta ile sehemu enzi zetu ilikuwa ikiitwa Mwembe Togwa.
Kwa nini paliitwa MWEMBETOGWA?
Kwa sababu, kwanza palikuwa na mwembe mkubwa pili, pakiuzwa togwa fulani maridadi sana.
Vijana wengi wa Dar es Salaam kipindi kile tulipenda kwenda pale kujiburudisha na kinywaji hicho murua.
Haya sasa nadhani mmefahamu kuwa pale FAYA palikuwa pakiitwa MWEMBETOGWA.




No comments:
Post a Comment