ADVERTISE WITH US

JE WAJUA MNAZI MMOJA ZAMANI PALIITWAJE



Unajua kwamba eneo la MNAZI MMOJA Dar es Salaam miaka ya 1960-1970 lilikuwa maarufu kwa jina la TUA TUGAWE?



Unajua jina hilo lilipatikana vipi?

Jina hilo lilitokana na uwepo wa wababe wa mji enzi hizo katika eneo hilo ambao walikuwa wakiwasubiri kina mama wanaopeleka vyakula kwa mafundi na kuwapora.

Kina mama walipofika maeneo yale na vyakula vyao waliambiwa "Hebu TUA TUGAWE". Jamaa walijipakulia vyakula vyao kisha kuwaachia kina mama vilibyobaki.

No comments: