Wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaifahamu barabara hii (Bibi Titi Road) kutokana na umaarufu wa Bibi huyu ambaye alikuwa miongoni mwa kina mama wachache walioshiriki katika harakati za Uhuru wa Tanganyika na baadae Tanzania.
Barabara ya Bibi Titi si maarufu kwa wenyeji tu bali hata wageni ambao mara kwa mara huipita kuelekea mahotelini.
Lakini je, wengi wetu tunafahamu barabara hii ilikuwa ikiitwaje hapo awali kabla ya kuitwa jina hili? Nadhani ni wachache sana wanaofahamu.
Barabara hii kabla ya kuitwa Bibi Titi Mohammed Road ilikuwa ikijulikana kama UWT Road.
UWT ni kifupi cha Umoja wa Wanawake (wa CCM) Tanzania.
Fahamu hilo kuanzia leo kuwa Bibi Titi Road ilikuwa ikiitwa UWT Road.
Karibu tukujuze.







No comments:
Post a Comment