ADVERTISE WITH US

JE UNAFAHAMU NENO KURASINI LILIZALIWAJE?

UNAFAHAMU NENO KURASINI LILIZALIWAJE?

Kurasini ni miongoni mwa maeneo maarufu ya jiji la Dar es Salaam.

Jiji la Dar es Salaam ni maarufu sana kwa shughuli za kibiashara kwa nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika.



Eneo la Kurasini lenyewe limekuwa maarufu zaidi kutokana na uwepo wa Bandari na Bandari Kavu ama maeneo ya kuhifadhia makontena.

Lakini licha ya umaarufu huo, ni watu wangapi wanafahamu jina Kurasini lilivyozaliwa?

Kona ya Wahenga tunakujuza hapa jinsi jina Kurasini lilivyozaliwa.

Kurasini inatokana na neno "Cool Ras Inn."
Cool Ras Inn lilikuwa ni jina la sehemu ya watu kustarehe baada ya harakati za kutwa nzima za kuujenga uchumi na hasa watu weupe.

Eneo hili la starehe liliitwa hivyo kutokana na eneo lenyewe kwa ujumla kuwa na sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (Tazama kipande cha ramani)

Wakazi wengi wa eneo hili walishindwa kutamka "COOL RAS INN" na hivyo wakatamka KURASINI.

Upungufu huo wa utamkaji ulishika hatamu mpaka eneo lote likajulikana kama Kurasini.

Karibu tukujuze.

CHANZO:Kona ya Wahenga.

No comments: