Google hivi karibuni waliingiza sokoni matoleo yao mapya ya simu za
Google Pixel 2 na Pixel 2 XL
ikiwa ni muendelezo wa toleo la Google Pixel na Pixel XL yaliyotoka
mwaka jana. Sasa nakuchambulia machache ambayo unaweza kukutana nayo
pindi utakapo kuwa tayari kununua simu hii.
Simu hizi zina muonekano mzuri na wa kipekee, Google wameamua
kuifanya iwe simu simple, ikiwa material ya Aluminium lakini ukiishika
unaweza kusema kuwa imeundwa kwa plastiki, Google wamejaribu kuifanya
simu iweze kushikwa vizuri kwa kuongeza material ya plastiki lakini
ukweli ndiyo huo imeundwa kwa Aluminium.
- YALIYOMO KWENYE SIMU HIZI.
Simu hizi zinakuja zikiwa na Specifications bomba kwani zinatumia Processor ya
Qualcomm Snapdragon 835 kama kwenye Samsung Galaxy S8, zinakuja zikiwa na Ram ya
4GB, uhifadhi wa ndani wa
64GB, kwenye upande wa betri kuna mabadiliko kwani PIXEL 2 ina ukubwa wa betri la
2700 MAH, na PIXEL 2 XL ina ukubwa wa betri
3520 MAH.
Google Pixel 2 ina kioo chenye ukubwa wa inch 5 na Google Pixel 2 XL
ina kioo cha ukubwa inch 6, na zote zinatumia teknolojia ya Gorilla
Glass.
Hii ndiyo sehemu ambayo watu wengi wamekuwa wakifatilia sana, na hapa
Google Pixel 2 na Pixel 2 XL wamefanya vizuri japokuwa hizi simu zote
hazina Camera mbili kwa nyuma (Dual Camera) kama yalivyo matoleo mengi
simu janja siku hizi badala yake kuna kinaitwa Dual Pixel kwenye Camera.
Google Pixel 2 na Pixel 2 XL zote zimewekwa Processor maalum kwa
ajili ya picha hivyo kuifanya simu hii kuwa nzuri sana kwenye kupiga
picha.

Simu zote hizi zina 12-MegaPixel dual-pixel nyuma na Camera ya mbele ina 8-MegaPixel.
Tizama picha zilizopigwa na hizi simu hapa.
- AI na MFUMO WA UENDESHAJI.
Ninapo zungumzia AI nazungumzia Artifical Intelligence na
tunazungumzia Google Assistant, unaweza kutumia msaidizi wa Google
kuiamrisha simu yako kufanya kile unachotaka kama kupiga simu, kutuma
SMS na mengine, jambo lingine jipya ni
ACTIVE EDGE teknolojia
mpya ambayo inakuwezesha kubinya simu yako ili uweze kutumia Google
Assistant, utalazimika kuset Active Edge kwenye simu yako ili uweze
kutumia.
Active Edge.
Simu hizi zinatumia mfumo wa uendeshaji wa
Android 8.0 (Oreo)
Hayo ni machache nimekugusia kuhusu simu hizi mbili, jambo
lingine la kufahamu ni bei ya simu hizi, Google Pixel 2 inaanza kuuzwa
kwa dola za kimarekani $649, na Google Pixel 2 XL inaanza kuuzwa kwa
$849
No comments:
Post a Comment