WhatsApp wameeleza programu hiyo itakuwa mahususi kwenye kuhakikisha mtumiaji anapata taarifa kama uthibitisho wa bidhaa, Ratiba za ndege, na vingine vingi. Mpaka sasa kampuni ya kwanza kuthibitishwa kwenye Programu ya WhatsApp for Business ni kampuni ya ndege ya KLM na mpaka sasa wateja wa shirika hilo la ndege wataweza kuwalisiana na kitengo cha huduma za mitandao ya kijamii na kupata taarifa kuhusu uthibitisho tiketi, ratiba za ndege, taarifa ya ndege na mengineyo kwa masaa 24.

Mpaka sasa WhatsApp hawajaeleza ni lini hasa App hiyo itaanza kupatikana, ila tunatambua kuwa wenye biashara ndogo ndogo wataweza kuipata bure na kampuni kubwa zenye watumiaji duniani kote wataweza kuchangia kiasi cha pesa ili kuweza kupata huduma kubwa zaidi.It's official: KLM is the first airline on WhatsApp with a verified account! Are you on board? pic.twitter.com/Kbilo3kL5Z— Royal Dutch Airlines (@KLM) September 5, 2017



No comments:
Post a Comment