ADVERTISE WITH US

Wajue Wasanii kutoka Afrika waliotajwa kwenye tuzo za Grammy 2017

Wakati majina ya mastaa waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Grammy 2017 yametoka, Afrika inaingia kwenye headlines nyingine mwaka huu ambapo kwa mara ya kwanza wasanii kutoka Nigeria wametajwa kati ya wanaowania tuzo hizo.

Wizkid kutoka Nigeria ametajwa katika tuzo hizo kupitia wimbo wa ‘One Dance’alioshirikishwa na Drake kutoka kwenye albam yake ya Views ambayo ipo kwenye kipengele cha albam bora ya mwaka. Grammy ni moja ya tuzo zinazoheshimika sana duniani ikitajwa kuwa ni tuzo zinazompa msanii heshima ya milele kwenye kazi zake.

pia  Kutana na Farida Demola Seriki 'KAH-LO' @thatkahlo Mwafrika mwingine aliyetajwa kwenye Tuzo za Grammy 2017.
grammys
Kah-Lo ambaye anatokea nchini Nigeria, ametajwa kwenye kipengele cha Best Dance Recording kwa ngoma yake “Rinse & Repeat”.
.
Anaungana na WizKid ambaye pia ametajwa kwenye kipengele cha 'Album of The Year' kwa mchango wake kwenye album ya Drake 'VIEWS'.

No comments: