ADVERTISE WITH US

USIKU WA TUZO ZA EATV 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love alipokuwa akitoa shukurani zake mara baada ya kupokea tuzo yake ya heshima iliyotolewa na EATV.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akipongezwa na Mpenzi mara baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindiwa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Nandi Mwiyombela kutoka kampuni ya Vodaco Tanzania katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akitumbuiza katika tuzo hizo.
Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa EATV inayoandaa tuzo hizo.


Shuhudia orodha kamili ya wasanii watakao ‘perform’ na kuandika historia usiku huu : Darassa, Bill Nass (Tanzania) , Maurice Kirya (Uganda),Wahu kutoka Kenya. Lady Jaydee(Tanzania), Barnaba kutoka Tanzania. Vanessa Mdee, Shetta, Alikiba (Tanzania)
Licha ya wasanii wa muziki pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo dance kutoka kwa vijana walioshika nafasi tatu za juu katika mashindano ya Dance100 2016 yanayoendeshwa na EATV.
Wasanii hao wataangusha show ya nguvu kwa watu mbalimbali ambao wanaendelea kumiminika katika ukumbi huu.
dsc_0011
Baadhi ya wasanii wakiwa katika zuria jekundu muda huu
dsc_0022dsc_0019dsc_1060
Upande wa radio EAST AFRICA ikiwa live
dsc_1065
Watangazaji wa radio East Africa wakiwa live
dsc_1069
Watangazaji wa EATV wakiwa Live
dsc_0041dsc_1073dsc_1077dsc_1100whatsapp-image-2016-12-10-at-19-45-26
SOURCE: +Cathbert Kajuna 

No comments: