ADVERTISE WITH US

Whatsapp yazindua rasmi videocalls Katika Whatsapp Android


1479228076588.png
Habari,

Mtandao maarufu wa kijamii WhatsApp wenye watumiaji zaidi Ya bilioni moja Dunia umeanzisha huduma ya mawasiliano ya video call kwa watumiaji wa smartphone za Android, ios na Windows kupitia mtandao huu ambao pia ni maarufu miongoni mwa Watanzania wengi . Mmoja wa waanzilishi wa WhatsApp Bwana
Jan Koum akiongea Reuters amesema WhatsApp yenye uwezo wa kupiga "video call" itasambazwa kwenye nchi 180 duniani ndani ya masaa baada ya sherehe za ufunguzi huko India.

Watumiaji wa WhatsApp watakuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa "video call" kwa wawapendao popote ulimwenguni. Nadhani itakuwa jambo nzuri sana la kustaajabisha."Imagine" upo nyumbani Tanzania na unawasiliana na bibi au babu aliye kijijini moja kwa moja kwenye video call au unawasiliana na mwanao aliye mbali na wewe kwenye masomo ndani au nje ya nchi.

Ijapokuwa WhatsApp siyo mtandao wa kwanza kutoa huduma hii kuna mitandao (app) mingine kama vile Google Duo,Skype na BBM kwa kutaja michache ambayo tayari inatoa huduma hii kwa kipindi kilefu sasa lakini bado kitendo cha WhatsApp cha kuanzisha huduma hii ni cha kupewa pongezi sana kwa kuwa WhatsApp ina watumiaji wengi wa kudumu na ni rahisi kuitumia ukilinganisha na mitandao mingine inayotoa huduma kama hii, hivyo watu wengi watanufaika na huduma hii muhimu. 

1479228164896.png 
Itakuwa ni rahisi kuwasiliana na umpendaye kwa "WhatsApp video call" utachotakiwa kufanya ili kuwasiliana kwa "video call" ni kufungua chat kwenye "app" yako ya WhatsApp kwenye Smartphone yako na huyo unayetaka kumpigigia halafu pofya sehemu ya kupiga simu alafu chagua video call bofya video call alafu subiri mwenzio apokee, hivyo tu alafu mambo yanakuwa safi mkiwa mubashara.

Wakati huo huo kuna habari nzuri pia kwa wamiliki na watumiaji wa simu za Blackberry 10 na Windows mobile 7 pamoja na Nokia symbian S60 kwamba wameongezewa muda wa kuendelea kutumia WhatsApp mpaka July 2017.