ADVERTISE WITH US

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA TIMU YA CHAPECOENSE YA BRAZIL IMEPATA AJALI NCHINI COLOMBIA,WATU 76 WAMERIPOTIWA KUPOTEZA MAISHA


Kikosi cha timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil wamepata ajali ya ndege wakiwa angani kuelekea kutua katika uwanja wa Medellin.
Ndege hiyo kabla ya kuanguka katika milima ya Colombia ilianza kupotea katika rada, ndege hiyo ya shirika la ndege la Airline LaMia imethibika kuwa ilikuwa imebeba abiria 72 na wafanyakazi 9 wa ndege, abiria hao 72 wanaripotiwa wote walikuwa ni msafara na wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil .

Habari za kusikitisha katika ulimwegu wa soka ni kwamba, klabu ya Chapecoense ya Brazil imepata ajali baada ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji pamoja na viongozi kuanguka kwenye mji wa Medellin, Colombia.
Chapecoense ilikuwa imefika hatua ya fainali ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Europa League kwa Ulaya na walikuwa wanaelekea Medellin kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa fainali dhidi ya Atletico Nacional siku ya Jumatano.
Mechi hiyo tayari imeshaahirishwa huku shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South American Football Confederation) limethimitisha kuahirisha shughuli zote kuhusiana na mchezo huo hadi watakapotoa taarifa baadae.



TRAGIC NEWS





SHOCKING

The first images of the plane (via @Oscar_Patinopic.twitter.com/9fs6Yb6YXU


BBC wameripoti kwamba, taarifa za ajali hiyo bado zinachanganya lakini inaripotiwa kuna watu ambao wapo hai.
Kwa upande wao Globo wameripoti kuwa, kulikuwa na abiria 72 pamoaja na wafanyakazi 9 wa ndege hiyo.

No comments: